Monday, November 16, 2015

WALIOFUKIWA NA VIFUSI MGODINI KWA SIKU 41 WAKUTWA HAI *PICHAZ*


BADRA
Ofisa Habari wa Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud.
MACHIMBO (1) MACHIMBO (2) MACHIMBO (3) 
MACHIMBO (4)
Manusra hao wakiendelea na matibabu.
WATU watano waliokuwa wakichimba madini katika mgodi wa Nyangarata uliopo Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wamepatikana wakiwa hai baada ya kufukiwa na vifusi kwenye mashimo ya mgodi huo kwa siku 41.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Ofisa Habari wa Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud amesema kuwa wachimbaji hao wanaodaiwa kuwa sita, walifukiwa na vifusi mnamo Oktoba 5, mwaka huu na kuendelea kuishi kwenye mashimo hayo huku wakila magome ya miti na udongo baada ya kushiwa chakula walichokuwa nancho, hadi jana Novemba 5, walipookolewa umbali wa kilomita 10 ndani ardhini na watano kati yao kukutwa hai huku mwenzao mmoja akidaiwa kufariki dunia.
Baada ya kupatikana wakiwa hai, manusra hao walikimbizwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya Kahama ambako wanaendelea kupata matibabu.
Badra amewataja waliopatikana hai kuwa ni; Joseph Bulule, Chacha Wambura, Unyiwa Aindo, Msafiri Gerald na Muhangwa Amos. Wakati aliyefariki akimtaja kwa jina la Mussa Supana.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI