Monday, November 16, 2015

TIMU YA TAIFA YA ZANZIBAR YAKABIDHIWA VIFAA VYA MAZOEZI NA KATIBU MKUU

Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Mhe Ali Mwinyikai akizungumza na Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar alipotembelea timu hiyo wakati wa mazeiai yao katika Uwanja wa Amani Zanzibar na kukabidhi vifaa vya mazoezi kwa ajili ya timu hiyo inayojiandaa na Michuano ya Chalenji Nchi Ethiopia mwezi huu.
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo  Mhe Ali Mwinyikai wakati alipofika kuitembelea timu hiyo ikiwa katika mazoezi ya kujiandaa na Michuano ya Chalenji yanayotarajiwa kufanyika mwezi huu Nchini Ethiopia.
Jopo la Viongozi wa Timu ya Taifa ya Zanzibar wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Mhe Ali Mwinyikai alipoitembelea timu hiyo ikiwa katika mazoezi katika uwanja wa Amani Zanzibar.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Mhe Ali Mwinyikai akimkabidhi seti za viatu Mjumbe wa Kamati ya Tendaji ya ZFA Hashim Salum vifaa hivyo kwa ajili ya wachezaji wa Timu ya Taifa kwa ajili ya mazoezi yao ya kujiandaa ni Michuano ya Chalenji  yanayotarajiwa kufanyika mwezi huu Nchi Ethiopia.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Dk Ali Mwinyikai akimkabidhi vifaa vya michezo Mipira na viatu vya mpira kwa ajili ya mazoezi ya Timu ya Taifa ya Zanzibar, Mjumbe wa Kamati Tendaji ya ZFA Hashim Salum, makabidhiano hayo yamefanyika katika uwanja wa Amani Zanzibar wakati wa mazoezi ya timu hiyo
Mjumbe wa Kamati Tendaji ya ZFA Hashim Salum akitowa shukrani kwa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo kwa msaada wao kwa Timu ya Taifa ya Vifaa vya mazoezi kwa ajili ya wachezaji hao na kuahidi kufanya vizuri na kurudi na Kombe la Ubingwa wa Chalenji mwaka huu.

Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar wakiwa katika uwanja wa amani baada ya kukabidhiwa vifaa vya mazoezi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Ali Mwinyikai
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar wakiwa katika uwanja wa amani baada ya kukabidhiwa vifaa vya mazoezi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Ali Mwinyikai

0 comments:

Post a Comment