Monday, November 16, 2015

SAMWEL SITTA ATOSWA USPIKA BUNGE LA 11


MKONGWE wa siasa ambaye aliyekuwa Spika wa bunge la tisa, Samuel Sitta ambaye alikuwa wakiwania nafasi ya uspika katika Bunge la 11, Kamati Kuu ya (CCM) imelikata rasmi jina lake licha ya kufanya kampeni mapema juzi kwenye viwanja vya Bunge.
Akitangaza majina yaliyopitishwa na kamati kuu Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema katika halmashauri hiyo imeyapitisha majina matatu ambayo ni Job Ndugai, Abdullah Ally Mwinyi na Tulia Akson.
Nape amesema kesho saa nne asubuhi majina hayo yatapelekwa yawasilishwa kwa wabunge wa CCM kwa ajili ya kupitisha jina la mgombea mmoja ambaye atagombea nafasi hiyo na wakambi ya upinzani.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI