Tuesday, September 15, 2015

UKAWA WAONGEA NA WAANDISHI WA HABARI USIKU HUU

UPDATES:
Mbatia analalamikia vitisho vya Mgombea wa CCM, Magufuli kuwa wakiwachagua wapinzani nchi itaingia kwenye machafuko
Mbatia: Watu wameanza kupoteza maisha, wana UKAWA wanadhalilishwa na wengine kutekwa
Mbatia: Hali imeanza kuwa tete, vitisho vya kila aina vimeanza. Tumedhalilishwa sana, tumeitwa matusi ya kila aina.
Mbatia: Lowassa si mdini, alikuwa anataka watanzania wamwombee. Mhe. Lowassa hajaenda kwenye nguvu za giza. Hajatumia viungo vya albino, ameenda kuomba viongozi wa dini wamwombee; udini wake unatoka wapi?
Mbatia: Tunawashukuru Lowassa na Sumaye kwa nia zao njema kuja Upinzani kuongeza nguvu ili tuyafanye mabadiliko ya kweli
Mbatia: Hata CCM wangemweka malaika, si rahisi kupata mabadiliko bila kufanya mabadiliko ya mfumo.
Mbatia: CCM wanasema usichague chama, chagua mtu. Watanzania wanatakiwa kujua kuwa Magufuli ni CCM, na hawezi kujitenganisha na CCM. Huwezi kulisukuma gari ukiwa ndani yake, lazima utoke ndipo ulisukume. Mabadiliko ndani ya CCM hayawezekani
Mbatia: Tumefanya utafiti, tuna uhakika wa ushindi mwaka huu
Mbatia: Hatutawapa CCM nafasi ya kufanya machafuko ndani ya Taifa hili
Mbatia: CCM hawana hati miliki ya kuitawala Tanzania hii. Watupishe tufanye mabadiliko haya kwa utulivu na amani.
Mbatia: Sumaye, Lowassa wana uzoefu mkubwa wa kuongoza Serikali, uwezo tunao! Tunao kina Mungai, Msindai, Mgeja n,k na wanao uzoefu wa kuongoza Serikali.
Mbatia: Limeibuka suala la ukabila. Ni aibu iliyoje? CCM wanahubiri ukabila, ukanda bila aibu yoyote!
Mbatia: Ilani ya Uchaguzi ni mkataba kati ya mpiga kura na mpigiwa kura; tuwaulize CCM Ilani yao iliyopita imetekelezwa kwa kiasi gani kabla hawajaja na ilani mpya. UKAWA tunayo ilani ya pamoja
Mbatia: Tunawataka CCM waje tufanye midahalo kwa hoja
Mbatia: Wenyeviti wa vyama wawekwe kwenye midahalo ili UKAWA tupambane na CCM kwa hoja na watanzania wajue pumba na mchele
Mbatia: UKAWA ipo imara, haitasambaratika!
Mbatia anafafanua wapi watapata fedha za kufanikisha yale wanayoahidi kwenye kampeni.
Mbatia anadai Safari za Rais hazikuwa na tija kwa Taifa.
Mbatia: Lowassa na Serikali yake wakiingia madarakani wanao uwezo wa kupunguza kodi kwa wafanyakazi
Mbatia: Tukinyimwa haki yetu kwa mbinu chafu… Hatutaki kuona yaliyotokea Kenya yakitokea Tanzania
Prof. Baregu ametoa ufafanuzi juu ya gharama za safari za JK na athari zake kwa Taifa (pamoja na gharama za kuingilia shughuli za watendaji walio chini yake na kutokuwepo kwake nchini)
Shaweji Mketo (CUF) pia ameendelea kuongelea safari za JK na athari zake kwa Taifa; amegusia pia chaguzi zilizofanywa jana na vikao vingine vya kiutendaji vinavyofanywa na Rais Kikwete nyakati hizi.
Mbatia kahitimisha kwa kusema "Tanzania bila CCM Inawezekana"
Asanteni

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI