Tuesday, September 15, 2015

AJALI POPOTE: BOSS WA BMW AANGUKA MBELE YA WAANDISHI WA HABARI *PICHAZ*

Ajali popote, ukiangalia pichaz na video za hii stori utaamini kwamba ajali haichagui mahali kwa kutokea… Boss wa Kampuni ya Magari ya BMW, Harald Krueger alijikuta akianguka kwenye stage mbele ya Camera za Waandishi wa Habari wakati alipokuwa akizungumzia ishu ya maonesho ya magari yao ambayo Kampuni hiyo itafanya Ujerumani!!
Msemaji wa Kampuni ya BMW, Maximilian Schoeberl amesema Boss wao haumwi na wala hana tatizo lolote, amekuwa mtu wa kusafiri sana kwa hiyo kuanguka kwake kunatokana na uchovu wa safari zake  za kikazi na kuna wakati hata Daktari wake alimwambia apunguze safari ili apate na muda wa kupumzika pia.
Hizi ni picha, mwanzo mpaka mwisho, CEO  Harald Krueger alivyokosa nguvu na kuanguka Jukwaani, Frankfurt Ujerumani.
 Mwanzo ilikuwa hivi, Boss anaendelea na kutambulisha Gari zao mpya… alikuwa poa kabisa yani.
Mara akayumba kama anarudi nyuma, akaishiwa nguvu mpaka akafika chini.
BMW CEO Harald Krueger faints during the BMW presentation on the first press day of the Frankfurt Auto Show in Frankfurt, Germany, Tuesday, Sept. 15, 2015. (Uli Deck/dpa via AP) 
Mwisho akafika chini kabisa !! BMW CEO Harald Krueger gets support after collapsing during the BMW presentation on the first press day of the Frankfurt Auto Show IAA in Frankfurt, Germany, Tuesday, Sept. 15, 2015. The car show runs through Sept. 27. (AP Photo/Jens Meyer) 
Baadhi ya wafanyakazi ilibidi wamfate haraka ili kumsaidia kuinuka.

CEO Harald Krueger aliinuliwa na ilibidi shughuli yenyewe aiachie hapohapo.
 Kipande cha Video nacho nimekipata hapa mtu wangu.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI