Tuesday, September 8, 2015

RAY C WA ‘KIUNO BILA MFUPA’ AREJESHA MWILI WAKE KWA KUPUNGUZA KG 30 *PICHAZ*

Ray C amefanikiwa kuurudisha mwili wake wa zamani ambao ulikuwa ni moja ya silaha zake awapo jukwaani, kutokana na wepesi wa kukizungusha kiuno chake kilichosababisha a.k.a ya ‘Kiuno bila mfupa’ kuanza kutumika.
ray cc
Jinsi Ray C alivyokuwa kabla ya kupungua
Toka Ray C ambaye jina lake halisi ni Rehema Chalamila aingie kwenye matatizo ya matumizi ya dawa za kulevya, mwili wake pia uliongezeka kwa kiasi kikubwa kiasi ambacho hata yeye binafsi amekiri kuwa alikuwa akiuchukia.
Ray c kiuno
Huyu ni Ray C wa leo baada ya kupungua
Baada ya kuanza mazoezi ya kupungua, Ray C amewa-surprise mashabiki wake kwa kupost picha mpya Instagram akiwa amefanikiwa kupungua kg 30 na kuandika;
“THE OLD RAY C IS BACK!!!!RAYC WA ZAMANI ANARUDI!!!!NAISHIA HAPA!SIKUTAKA KUWAONYESHA JINSI GANI NILIVYOKUWA NAJICHUKIA NIKIJIANGALIA KWENYE KIOO NA UNENE NILIOKUWA!MTU NILIEKUWA NAMTEGEMEA KUNISAIDIA KUNIRUDISHA KWENYE MUZIKI ALIUCHUKIA SANA UNENE WANGU NA AKANIAMBIA KAMA NATAKA NATAKA KURUDI KWENYE GAME NIPUNGUE KILO 30!!!!!!
NINA FURAHA YA AJABU KUMUONA TENA RAY C YULE NILIOMZOEA!!NAANZA SHOOTING NEXT WEEK!!!YEI YE!I!!”
rayc

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI