Monday, September 7, 2015

MWIGIZAJI JIM IYKE APATA MTOTO…!

Mwigizaji wa Nollywood Nigeria Jim Iyke ana sababu kubwa sana ya kutabasamu na kufurahi siku ya leo. Baada ya kumpoteza mama yake mzazi kipindi kama hiki mwaka jana staa huyo wa movie anafungua ukurasa mpya wa furaha maishani mwake.
jim-iyke2
Jim Iyke na mpenzi wake.
Jim Iyke na mpenzi wake wa mwaka mmoja wamemkaribisha duniani mtoto wao wa kwanza wa kiume kwenye hospitali ya Grady Hospital iliyopo jijini Atlanta Marekani.
Jim-Iyke
Jim Iyke alikuwa na haya ya kusema kuhusu baraka za kupata zawadi ya mtoto mwaka huu..
>>>“Ni mwaka jana tu nilikuwa na huzuni mkubwa baada ya kumpoteza mama yangu mzazi lakini leo, mwaka mmoja badaae nina machozi ya furaha”. <<< Jim Iyke.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI