Tuesday, September 15, 2015

AUNT EZEKIEL AFUNGUKA HAYA, KUHUSU KUONDOKA UKAWA KUHAMIA CCM….!! *PICHAZ*

.
Ni stori inayoendelea kuchukua healines kwenye mitandao mbalimbali kuhusu Aunt Ezekiel na Vicent Kigosi, sasa leo Sept 15, 2015 ripota wa millardayo.com alikutana na Aunt Ezekiel na kueleza sababu zilivyomfanya yeye kuhama UKAWA na kuhamia chama cha Mapinduzu.
Msanii huyo alipokutana na ripota wa millardayo.com alithibitisha na kusema..’Kweli nimetoka Ukawa na kuhamia CCM hayani maamuzi yangu binafsi ambayo nimeyafanya baada ya kukaa na kufikia kwamba Magufuli ndio anafaa kuwa Rais wangu kwasababu ni mtu ambaye anakupa sera ambazo zinaeleweka anakuambia kabisa hapa ni kazi na ukiangalia je ni kwanini anasema ni kazi hakuna mabadiliko yanayotokana na kazi‘ – Aunt Ezekiel
‘Lazima ufanye kazi ili upate mabadiliko kwa hiyo nimeona ni vema niungana na hawa wanaofanya kazi ii kutetea mabadiliko kuliko kuhitaji mabadiliko bila kufanya kazi naamini huku ambapo nimerudi nitapata mabadiliko yakutosha kupitia kazi nitakazofanya’- Aunt Ezekiel

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI