Wednesday, August 19, 2015

SHAMBULIO LA SYRIA LAUA WATU KUMI *PICHA*

Kobane, Syria ikifumuliwa kwa mripuko.
********
Shambulio la bomu lililotekelezwa kwenye kikosi cha ulinzi cha wakurdi kaskazini mashariki mwa Syria limetaarifiwa kuua watu wapatao kumi.
Makao makuu ya masuala ya Haki za Binadamu ya nchi hiyo yalioko nchini Uingereza yamesema mlipuko huo ulilenga kulipua makao makuu ya wakurdi katika mji wa Qamishli .
Hata hivyo vikosi cha kikurdi vimejipanga kukabiliana na wanamgambo wa dola ya kiislamu , ambacho mara nyingi hufanya mashambulizi ya aina hiyo.
Wakati huo huo,umoja wa mataifa umesema Syria linakabiliwa na homa ya matumbo katika kambi ya wakimbizi ya Yarmouk ambayo ipo kwenye vitongoji vya Syria ndani ya mji mkuu wa Damascus.
Msemaji wa umoja wa mataifa amesema kuwa ugonjwa huo umshamiri katika kambi hiyo ya wakimbizi yapata miezi sita sasa.inaelezwa kuwa Yarmourk ni eneo ambalo linakumbwa na majanga kila mara .

Ingawa eneo hilo liko chini ya himaya ya serikali tangu mwaka 2013 lakini bado hali imezidi kuwa tete tangu kikosi cha wanamgambo wa dola ya kiislamu IS walipowavamia katika kambi hiyo na kuangamiza watu.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI