Friday, August 14, 2015

NORA: WASANII WANAOTUMIKA KISIASA! HAWAITAMBUI THAMANI YAO...KILA MWAKA WANATUMIKA NA KUACHWA SOLEMBA!

Nora wa Bongo Movies
Msanii wa ‘long time’ kwenye ulimwengu wa filamu, Nuru Nassoro ‘Nora’ amewananga wasanii ambao wanakubali kutumika kisiasa katika kipindi hiki bila kujua madhara watakayopata baada ya uchaguzi.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Nora alisema kuwa, anawashangaa baadhi ya wasanii kukubali kununulika wakati wakijua kuwa, baada ya uchaguzi watamwagwa.
“Jamani mimi nashangaa kuona wasanii tunatumika kwa kiasi hiki, thamani yetu hatuitambui kabisa, kila baada ya miaka mitano tunatumika kisha tunaachwa solemba, yaani dah!” alisema Nora.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI