Saturday, August 15, 2015

NE-YO KUTUMBUIZA COKE STUDIO AFRICA NCHINI KENYA NA NYOTA WA AFRIKA

Kufuatia tetesi mbalimbali kuhusu ujio wa mkali wa miondoko ya R&B na Pop NE-YO katika onyesho la Coke Studio Afrika msimu wa tatu, sasa imethibitishwa kuwa msanii huyo atakuja rasmi.

NE-YO ambaye atakuwa ndiye mgeni pekee kutoka nje ya Afrika, ataambatana na nyota wengine wa Afrika ambao ni Wangechi (Kenya), Alikiba  (Tanzania), Maurice Kirya (Uganda), Dama Do Bling (Mozambique) na Ice Prince (Nigeria) ambapo wataungana kufanya nyimbo moja.

Kuelekea ujio wake nchini Kenya, NE-YO  ametoa taarifa rasmi ambayo inasema, 
“ Ni heshima kubwa sana kwangu kurejea Afrika na kushirikiana na wasanii kutoka bara hili, kupitia Coke Studio Afrika, hii ni fursa nzuri inayojenga uhusiano mzuri miongoni mwa watu wa rangi , makabila na dini zote kujumuika kwa pamoja katika onyesho hili la kukumbukwa.. Nimefurahi sana kupata wasaa huu wa kujumuika na wasanii na wanamuziki hawa wenye vipaji vikubwa kabisa.

0 comments:

Post a Comment