Saturday, August 15, 2015

LOWASSA STOP!!! HAYA SASA CHEKI PICHA LILIVYOCHEZWA BAADA YA MSAFARA WA EL KUSIMAMISHWA!

Polisi mkoani Kilimanjaro wakiwa wameuzuia msafara wa Waziri Mkuu Mstaafu na Mgombea Urais kupitia Chadema na anaeungwa mkono na UKAWA, Edward Lowassa katika kijiji cha Maroro, Wilayani Mwanga mkoa wa Kilimanjaro, wakati anakwenda kuhudhuria mazishi ya Kada na Mwasisi wa Chama cha Mapinduzi CCM, mzee Peter Kisumo huko Usangi.

 Viongozi wa upinzani waliokua katika msafara huo.
 Msafara ukiwa umesimama


 Polisi wakiwa wametanda.
 Edward Lowassa akizungumza jambo.
 Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia akijaribu kuzungumza na Polisi.
 Mbatia akifafanua jambo kwa Wanahabari kuhusiana na zuio hilo la Polisi.
Lowassa akizungumza kwa simu huku akiwa na Mbunge wa Moshi Mjini Mzee Philemon Ndesamburo.
Edward Lowassa akizungumza na wanacham wa vyama mbalimbali waliojitokeza kumlaki na kumsimamisha katika eneo la Boma Ng'ombe
***************
Polisi mjini Mwanga, mkoani Kilimanjaro umezuia msafara wa mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa uliokuwa unaelekea Usangi kuhudhuria mazishi ya kada wa CCM, Peter Kisumo.
Vyanzo vya kuaminika toka mjini Mwanga vinasema, polisi walizuia msafara huo kutokana na kujumuisha idadi kubwa ya magari ya viongozi waandamizi wa Ukawa na wabunge wanaounda umoja huo jambo ambalo polisi hawakuafiki.
Taarifa zinasema, tukio hilo lililotokea katikati ya Mwanga na Usangi lilizusha mjadala wa zaidi ya dakika 30, polisi wakitaka Lowassa aende mazishini peke yake huku magari mengine yaliyoambatana naye yarejee yalikotoka jambo ambalo halikuafikiwa na mwanasiasa huyo.
Baada ya polisi kusisitiza kutoruhusu msafara mzima uende mazishini mgombea huyo aliamua yeye na maofisa wengine alioambatana nao kurudi Mwanga akisisitiza asingeweza kwenda peke yake akiwaacha watu aliambatana nao.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI