TIMU ya taifa Intamba Murugamba kutoka Burundi inajiandaa vilivyo kwa wiki ya pili sasa katika mechi za mtoano ya kufudhu CAN 2017 nchini Gabon. Intamba Murugamba ipo kwenye maandalizi kwa pambano watakayo karibisha timu ya taifa ya Niger tarehe 5 septemba mjini Bujumbura kwenye uwanza wa mwana mfalme Prince Louis Rwagasore.
Orodha ya wachezaji wakulipwa wamefahamika baada tu ya kamati nzima na kocha kuweka wazi orodha ya wachezaji ambao wanacheza mpira wakulipwa nje ya nch ya Burundi ambao watakuja kujiunga na wachezaji wa nyumbani. Orodha iyo imekuwa inasubiriwa sana na mashabikiwa wa timu ya taifa uku wakishangazwa sana na kutokuona jina la nahodha wa zamani wa timu ya taifa Saido Ntibazonkiza ambaye anacheza Uturuki katika klabu ya Akhisar. Saido ni mchezaji wa kwanza kupendwa sana na mashabiki wa Burundi kwakua yeye ndiye mchezaji bora na mchango wake kwenye timu ya taifa ni kubwa zaidi uku tukimaanisha uwezo wa ndani na nje pia uwanjani. Saido ameshtumiwa na kocha mkuu wa Burundi Bwana Abdel Malek kwa ukosefu wa adabu alio onesha mbele ya kocha na mbele ya wachezaji wenza tangu siku ya mechi ya kirafiki dhidi ya Iles Maurices.
Saidi Ntibazonkiza |
Watu wanashangazwa sana kuona tatizo hili imekosa suluhu na wanaofia tena kwa kumkosa Saido kwenye mechi dhidi ya Niger itakua ni pengo kubwa sana kama ilivyo kuwa mechi ya awali dhidi ya Senegale (3-1). kwa habari tulizopata ni kwamba tayari timu ya taifa Intamba Murugamba imekwisha pata mchezaji atakae murudilia Saido na ikiwezekana akachukuwa na namba 10 ili awakilishe Burundi vizuri. Mchezaji ambae anasubiriwa kwa amu sana ni Nzeyimana Jean kwajina maarufu Juhainy Johane kutoka katika klabu ya Chibuto uko Mozambike. Nzeyimana Jean ama Johane, ni mchezaji muzuri sana na mashabiki wa timu ya taifa walipo sikia wito wake basi moja kwa moja wamepunguza asira yao ya kumtegea Saido na wote kwasasa wameweka matumaini yao kwa mchezaji mrundi Jean Nzeyimana. tuwakumbushe kuwa itakua ni mara ya kwanza Johane kuichezea nchi yake ya Burundi. Jean Nzeyimana amewahi kucheza Ureno (Portugal) katika klabu ya Pacos Fereira na baadae kusajiliwa na Chibuto ya Mozambike.
Jean Nzeyimana a.k.a Juhainy Johane |
upande mwingine ni wa golikipa Nzokira Jeff kutoka katiaka klabu ya Telecom Djibouti ya nchini Djibouti, naye pia ameitwa na kwasasa amekwisha anza mazowezi na timu ya taifa uku wakisubiria wengine kutoka nchi mbalimbali kuwasili Burundi na kuunda timu nzito.
hii ndio kwa ufupi orodha ya wachezaji walio itwa na kamati la shirikisho la mpira Burundi
Habarugira David (Fc Trond/Ubeljiji), Ndikumana Yamin Selemani ( Deportivo de primeiro de Luanda/ Angola), Fiston Abdoulazak ( Mamelodi Sundowns/ Afrika Ya Kusini), Kavumbagu Didier ( AZAM /Tanzania), Cedrik Amissi ( Chibouto/Mozambique), Nzeyimana Jean a. k. a Juhainy Johane( Chibouto/Mozambique), Nimubona Emerry Kadogo ( Simba Sc/Tanzania), Foadi Ndayisenga( Sofapaka/ Kenya), Frederick Nsabiyumva( Jomo Cosmos/Afrika Kusini), Pierron Kwizera ( Rayon Sport/Rwanda), Papy Faty ( Bidvess University/ Afrika Kusini) Kalim Makenzi (Gor Mahie/Kenya), Nzokira Jeff ( Telecom Djibouti/Djiboutie).
0 comments:
Post a Comment