Sunday, February 1, 2015

MTOTO WA WHITNEY HUSTON AENDELEA VIZURI BAADA YA KUANZA MATIBABU *PICHAZ*

MTOTO wa aliyekuwa mwanamuziki maarufu nchini Marekani Whitney Huston, Bobbi Kristina anaendelea vizuri na ameanza kupumua baada ya kupata matibabu.
Bobbi alitaarifiwa kuanguka  na kupoteza fahamu katika bafu nyumbani kwake siku ya Jumamosi.
Polisi nchini Marekani imesema kuwa mume pamoja na rafiki wa binti wa mwanamuziki huyo wa marekani amekutwa hana fahamu hivyo walilazimika kutoa taarifa polisi kabla ya kumfikisha hospitalini.
Msemaji wa polisi anasema kuwa wanachojua ni kuwa Bobbi bado ni mzima na anapumua hawana taarifa zaidi ya hapo kwani tukio hilo bado linafanyiwa uchunguzi.
Hospital ya North Fulton anakopatiwa matibabu mtoto wa mwanamuziki huyo hawajatoa majibu yeyote juu ya hali ya bobby.
Bobbi Kristina akiwa na mumewe.
Tukio hilo linakuja ikiwa ni wiki imebakia  kuadhimisha miaka mitatu tangu kifo cha mama yake whitney huston baada ya kukutwa hajitambui bafuni katika chumba cha hotel mjini Los Angels.
Bobbi Kristina

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI