Wednesday, February 11, 2015

MAGARI YASIO NA DEREVA KUENDESHWA UK 2017


MABADILIKO yatakayofanyiwa barabara kuu pamoja na majaribio yatasaidia katika kuyaendesha magari yasio na madereva katika barabara za Uingereza,ripoti ya idara ya uchukuzi imebaini.
Serikali inataka Uingereza kutambulika ulimwenguni kama kiongozia wa teknolojia ya magari yasiokuwa na dereva. Itachapisha sheria katika majira ya kiangazi ambayo itaruhusu majaribio ya magari hayo kuwa na uhuru wa kujiendesha. Serikali imeahidi kuangaziwa upya sheria zilizopo ifikiapo majira ya kiangazi ya mwaka 2017. magari yasiokuwa na dereva.
Mpango huo utabaini iwapo kiwango cha juu cha uendeshaji magari kitahitajika miongoni mwa magari yanayojiendesha. Pia sheria hiyo itaangazia ni nani wa kulaumiwa iwapo kutakuwa na ajali mbali na usalama wa madereva na watembeaji wa miguu.
Ripoti ya Idara ya usalama imekiri kwamba magari yanayojiendesha bila madereva huenda hayafuati maagizo na kwamba majaribio yanayoendelea yatahitaji kuwashirikisha madereva waliofuzu kuyaendesha magari hayo.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI