Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga Jerry Murro akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Unguja katika kambi ya timu yao iliyopo hoteli ya Zanzibar Ocean View.
********
KLABU ya Yanga imetengaza rasmi kuachana na mlinda mlango wake Juma Kaseja kwa madai kuwa Tanzania One huyo wa zamani hajaonekana klabuni kwa majuma matatu.
Mkuu wa Idara ya habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro amekutana na waandishi wa habari leo mjini Zanzibar na kueleza kuwa kitendo hicho cha Kaseja kimemfanya avunje mwenyewe mkataba wake na klabu hiyo yenye maskani yake makutano ya Twiga na Jangwani, Kariakoo, Dar es salaam.
Katika hatua nyingine, Yanga imekanusha madai ya kushindwa kumlipa Kaseja milioni 20 ambayo ni sehemu ya fedha za usajili wake wakidai walishamlipa kabla ya kupeleka barua ya madai.
0 comments:
Post a Comment