WANAWAKE wengine watatu Nchini Marekani wamejitokeza hadharani kuendeleza mashtaka yanayomkabili mchekeshaji wa siku nyingi nchini humo Bill Cosby.
Wanawake hao wamekiri kunyanyaswa kijinsia na muigizaji huyo katika kipindi cha mwaka 1981 hadi 1996.
Mchekeshaji Cosby mwenye umri wa miaka 77 anakabiliwa na mashtaka mbalimbali ya unyanyasaji wa kijinsia ikiwemo ubakaji pamoja na madawa ya kulevya katika miaka 1970 na kuendelea.
Wanawake hao watatu waliojitokeza mbele ya waandishi wa habari wamesema kuwa matukio ya unyanyasaji wa kijinsia dhidi yao yalitokea katika miji ya Los Angela na Las Vegas walipokutana katika kipindi chake cha The Cosby Show.
Mmoja wa wanawake hao anaejulikana kwa jina la Linda kirkpatrick anasema kuwa ameamua kujitokeza hivi sasa ingawa anahofia jamii inaweza isimuamini.
Mpaka sasa hakuna majibu ya haraka kutoka kwa wakili wa mchekeshaji huyo licha ya madai haya kushabihiana na mashtaka yaliyokuwa yakimkabili ingawa muigizaji huyo alikana makosa hayo.
0 comments:
Post a Comment