Saturday, January 3, 2015

MWAKA 2015 MAJANGA MATUPU: HUKU PANYA ROAD, HUKU KANGA MOKO…TUTAPONA KWELI?? *PICHAZ*

 NI matukio ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara ambapo wengi ni watu wanaoizunguka jamii yetu hii hii tunayoishi. Mbaya zaidi wanafanya matukio haya huku kukiwa na uwezekano mkubwa wa kuwachukulia hatua.
Wito umetolewa kwa vitendo hivi kukomeshwa, mwananchi chukua hatua ya kuripoti matukio kama haya.
Hebu msikilize Kamanda kova alichokisema kupitia TBC 1 juu ya panya Road:
"Tutashughulikia suala la ‘Panya road’ na leo doria inaendelea usiku kucha, wananchi waondoe hofu wajue jeshi la Polisi lipo… Haiwezekani panya road wakatawala Dar es Salaam… Haiwezekani panya road wawe na nguvu kuliko jeshi la Polisi…” Wamekamatwa wawili… tuliwakamata muda mfupi tu baada ya kuanza vurugu zao…”– Kamanda Kova.
Play halo chini Kumsikiliza Kamanda Kova…!
Vitendo kama hivi vya kingono pia vinafaa kupigwa STOP kwani vinahamasisha vijana kujiingiza katika vishawishi vinavyoweza kupelekea afya zao kuyumba kutokana na janga zima linaloiendesha dunia la UKIMWI.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI