Saturday, January 3, 2015

MSICHANA WA MIAKA 7 ANUSURIKA KATIKA AJALI YA NDEGE *PICHA*

Ajali ya ndege.
******
MTOTO mmoja wa miaka saba ametembea hadi katika nyumba moja katika jimbo la Kentucky nchini Marekani ili kuripoti kuanguka kwa ndege aliyoishuhudia.
Kulingana na polisi ndege hiyo baadaye ilipatikana imeanguka huku watu wanne wakiwa wamefariki katika kaunti ya Lyon yapata kilomita 50 mashariki mwa mji wa Paducah
Kituo cha runinga cha NBC nchini Marekani kimesema kuwa msichana huyo alimwarifu mtu aliyemfungulia mlango kwamba wazazi wake walifariki katika ajali hiyo ya ndege.
Picha ya ndege hiyo haijatolewa na polisi hawajatoa tamko lolote kuhusu uhusiano wake na waathirwa.
Shirika linalosimamia anga za juu limesema kuwa maafisa wanaodhibiti usafiri wa ndege walipoteza mawasiliano na ndege hiyo aina ya Piper PA-34 baada ya rubani kuripoti matatizo ya mitambo.

Dakika 30 baada ya ndege hiyo kupoteza mawasiliano ,mkaazi mmoja wa Lyon kaunti aliwapigia simu polisi kuwaarifu kuwa msichana huyo aliwasili katika nyumba yake ili kuripoti kuhusu ajali hiyo.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI