Sunday, January 4, 2015

LIVERPOOL WAMSAINISHA MKATABA NYOTA HUYU MKUBWA *PICHAZ*

BAADA ya kuwepo kwa tetesi nyingi zikimhusisha na kuwa mbioni kuihama klabu yake , Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Raheem Sterling anatarajiwa kutia saini mkataba mpya utakaomfanya aendelee kubaki na klabu hiyo kwa miaka mitano zaidi .
Kwa mujibu wa ripoti zilizotoka magazetini nchini England asubuhi ya leo (jumapili) , Sterling atatia saini mkataba huo ambao utamuingizia mshahara wa paundi 100,000 kwa mwezi akiwa amepandishiwa mshahara kutoka paundi 60,000.
Raheem Sterling atasaini mkataba mpya wa miaka mitano mwishoni mwa mwezi huu .
Hatua hii inakuja siku chache baada ya klabu ya Liverpool kutangaza kuwa nahodha wake wa muda mrefu Steven Gerard ataondoka klabu hapo mwishoni mwa msimu huu huku ripoti zikisema kuwa atakwenda Marekani .
Kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi zikimhusisha Sterling na kujiunga na klabu bingwa ya Ulaya Real Madrid na taarifa za Sterling kusaini mkataba mpya zitakuwa nzuri kwa mashabiki wa Liverpool katika kipindi hiki ambacho klabu hiyo itampoteza Gerard.
Mabingwa wa Ulaya Real Madrid waliripotiwa kuwa na mpango wa kumsajili Sterling.
Sterling atasaini mkataba huo mpya mwishoni mwa mwezi huu wakati ambapo mazungumzo na uongozi wa Liverpool yatakpokuwa yamekamilika na kutangazwa rasmi .

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI