Saturday, January 3, 2015

HUYU NDIYE KIPA BORA WA LIGI YA HISPANIA MPAKA SASA…! *PICHAZ*

claudio-bravo-siebtem-spiel-ohen-gegentor-01
Kipa wa Barcelona Claudio Bravo ameonekana kuwa kipa bora kwenye ligi ya Hispania msimu huu .
Kipa huyu ambaye yuko kwenye msimu wake wa kwanza akiwa amenunuliwa toka Real Sociedad kuziba pengo la Victor Valdez hadi sasa amecheza kwenye mechi karibu zote za ligi kuu ya Hispania huku akiwa na idadi ndogo ya mabao ya kufungwa tofauti na makipa wengine .
Mwanzoni mwa msimu kipa huyu alicheza jumla ya mechi nane mfululizo bila kuruhusu bao lolote .
Baada ya hapo alipatwa na mkosi baada ya kuruhusu mabao matatu kwenye mechi moja dhidi ya Real Madrid huku akiruhusu mabao mengine katika mechi tatu zilizofuatia .
Bravo alisajiliwa na Barcelona msimu huu akitokea Real Sociedad ya Hispania .
Hadi sasa akiwa amecheza kwenye mechi 16 za La Liga Bravo amefungwa mabao 7 pekee akiwa na watsani wa kufungwa bao 0.43 kwenye kila mechi wastani ambao hakuna kipa yoyote kwenye ligi ya Hispania amewahi kuwa nao.
Rekodi pekee bora kwa makipa nchini Hispania iliwahi kuwekwa na kipa wa Deportivo Francisco Liano ambaye katika msimu wa mwkaa 1993/94 aliruhusu mabao 18 tu kwenye mechi 38 za msimu mzima katika wastani wa bao 0.47.
Barcelona itauanza mwaka 2015 ikiwa kwenye nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ya Hispania pointi moja nyuma ya vinara wa ligi hiyo Real Madrid na mabingwa hawa wa zamani wa ulaya wakiwa chini ya Luis Enrique wanatarajia kuingia uwanjani hapo kesho kucheza na timu ya zamani ya Claudio Bravo Real Sociedad ambao kwa sasa wako chini ya kocha wa zamani wa Manchester United David Moyes kwenye mchezo wao wa 17 wa ligi ya Hispania .
Hadi sasa Bravo ameruhusu mabao 7 pekee kwenye mechi 16 za ligi ya Hispania.
Endapo Claudio Bravo ataendelea na kasi hii atamaliza msimu akiwa ameruhusu mabao 16 pekee na hivyo kuweka rekodi ya kuwa kipa aliyefungwa mabao machache kuliko wote katika Historia ya Hispania .

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI