Tuesday, January 6, 2015

HII NDIO HOFU ILIYOTANDA MANCHESTER UNITED

24696B3800000578-0-image-a-32_1420397606924
Beki wa Manchester United,  Rafael da Silva (kushoto) aliumia dhidi ya Yeovil.
*******
LOUIS van Gaal amekumbwa na majanga ya majeruhi licha ya Manchester United kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi yaYeovil Town katika mechi ya raundi ya tatu ya kombe la FA.
Rafael da Silva alivujika mfupa wa taya katika kipindi cha kwanza na kutolewa wakati wa mapumziko, wakati mlinzi mwenzake Paddy McNair alihitaji bandeji kichwani kufuatia kugongana na  Kieffer Moore.
Van Gaal pia alieleza kuwa beki mwingine Luke Shaw alipata majeraha mapya ya kifundo cha mguu na yeye alitolewa wakati wa mapumziko baada ya kucheza kwa kutumia dawa ya kuzuia maumivu.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI