Friday, January 2, 2015

ANGALIA VITUKO NA MBWEMBWE ZA WABONGO KATIKA FUKWE ZA BAHARI YA HINDI *PICHAZ*


Mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam walimiminika jana katika ufukwe wa Bahari ya Hindi eneo la Coco Beach kufurahia mwaka mpya wa 2015 kwa kuogelea.
Huku pakiwa na ulizni mkali wa Polisi, wakazi hao walionekana kufurahia mwaka mpya na familia zao kwa kugolea huku mawimbi yakiwa ni madogo jambo ambalo lilileta raha.
watoto walijiachia vilivyo katika maji...
Wapo waliojisikia raha kwa kutembea tu ufukweni...
Wavaa milegezo nao bado wapo 2015 na wao pia walikuwepo ufukweni.
Baharini kuna mengi, kijana huyu katika kupiga mbizi akachomwa na kitu, hapa mwenzake akimpa huduma ya kwanza.
Wapo waliyo yatafakari maji na kubaki wanayaangalia tu.
Huyu katika kuhofia usalama wa mali zaki bila ya kujua Polisi wapo aliingia majini na mizigo yake...

Polisi wakivinjari katika ufukwe huo wa Bahari ya Hindi.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI