Sunday, January 4, 2015

AMUUA MPENZI WAKE KWA KUMPIGA NA JIWE KICHWANI WAKIWA MATEMBEZINI BRAZIL

lesb
MWANAMKE mmoja Brazil amemuua mpenzi wake wa kike kwa kumpiga na jiwe kichwani wakati walipokua wakifurahia matembezi katika mji wa Ceara.
Mirium Franca mwenye miaka 29 amefunguliwa mashtaka ya kifo na polisi wa nchi hiyo kwa kitendo hicho cha makusudi bila kueleza sababu.
Mwili wa mwanamke huyo raia wa Italy ulikutwa na watalii katika makumbusho ya Jericoacoara ambapo walikwenda kutembea na ulionyesha umepigwa kwa kutumia kipande cha mwamba kichwani na kifuani.
“Siku moja kabla ya kifo cha Gaia Molinari aliniambia mikakati yake ya kutaka kuhamia nchini Brazil,lakini leo nimepata habari nyingine,”alisema mama yake mzazi Valentina Carraro

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI