Monday, December 29, 2014

VILIO NA HUZUNI: NCHI MBALIMBALI ZASAIDIA KUITAFUTA NDEGE ILIYOPOTEA *PICHAZ*

 Ndugu wa Abiria wakilia kwa uchungu
*******
NCHI mbalimbali za kimataifa zimejitolea kupeleka timu kusaidia kutafuta ndege ya Air Asia iliyoripotiwa kupotea dec 28  wakati ikitokea nchini Indonesia kuelekea singapore ikiwa na abiria 162 huku kiongozi mmoja wa juu akisema huenda ndege hiyo ikawa chini ya bahari.
Nchi hizo ni pamoja na Austaralia, singapore na Malaysia ambazo zimetoa ndege na meli katika kusaidia kutafuta ndege hiyo ambayo mpaka sasa haijafamika mahali ilipo.

Hata hivyo ndugu  na jamaa wa abiria waliokuwemo katika ndege hiyo wamekuwa wakisubiri taarifa kuhusiana na wapendwa wao kwa zaidi ya siku moja baada ya ndege hiyo yenye namba za usajili QZ8501 kupotea katika eneo la Java
Baadhi ya ndugu wa abiria wa ndege hiyo wamekesha usiku mzima katika mji wa Surabaya wakiwa na matumaini ya kupata taarifa za ndugu zo wakati timu za kimataifa zikiongeza juhudi za kuitafuta ndege hiyo
Vick Said ambaye ni mmoja wa ndugu wa abiria hao anasema bado hajakata tamaa kuwatafuta ndugu zake wawili waliokuwemo katika ndege hiyo  huku akitupa lawama kwa maafisa wa ndege hiyo kutotoa ushirikiano kwa wanafamilia katika tukio hilo la huzuni.
Ndege hiyo ambayo ilikuwa na abiria 162 kati yao 155 ni raia kutoka indonesia, watatu  kutoka  korea kusini na waliobaki ni kutoka Malaysia, Uingereza, na Ufaransa.
 Rubani wa Ndege Iliyopotea Ya Air Asia
 Ni vilio na Majonzi.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI