WAKAZI wa jiji la Dar es salaam wapo katika hatari ya kupatwa na
magonjwa makubwa kama saratani, utasa, kupoteza uwezo wa kuona,kuharibu
ubongo,maini na figokutokana na matumizi ya mboga za majani zinazolimwa
katika mabonde ya jiji.
Matumizi ya mboga hizo ni makubwa jijini humo,yakitokana na umuhimu wake
kwa afya za watu na hali duni ya maisha inazozifanya familia nyingi
kumudu gharama zake ikilinganishwa na vitoweo vingine.
Sehemu kubwa ya mboga hizo inatokana na kilimo kinachofanyika katika
mbonde la mto Msimbazi na maeneo ya Kigogo-Sambusa,Ubungo,Gereji
mchicha,Vingunguti na Tandale.
Katika Gazeti la NIPASHE limesema tayari matokeo ya tafiti kadhaa
yamedhihirisha maji yanayotumika kwa umwagiliaji wa mboga za majani
jijini humo kuwa na kemikali zenye sumu ama taka zinazotoka viwandani na
kwenye makazi ya watu.
Pili wakazi wanaoishi pembezoni mwa bonde la Msimbazi na maeneo mengine
yanayolimwa mboga hizo,wamebainika kutupa taka kama betri zilizoisha
muda wa matumizi,masalia ya simu za mkononi,vipuri vya magari na
majokofu mabovu.
Taka hizo zenye sumu zinatupwa kwenye mifereji ya maji yanayotumika kwa
umwagiliaji wa mboga hivyo kuzidi kuhatarisha afya za walaji.
Chuo Kikuu cha Ardhi kilifanya utafiti katika bonde la mto Msimbazi na
udongo na maji kwa vigezo vya Shirika la Afya dunia WHO na Shirika la
viwango nchini TBS.
Akizungumzia utafiti huo mhadhiri wa Uhandisi wa Mazingira kutoka Chuo
kikuu cha Ardhi ‘Aru’ Willium Mwagoha alisema waligundua mabwawa ya
majitaka yanayotoka mabibo, dampo la vingunguti, viwandani na gereji
mbalimbali yanamwaga maji kwenye mto huo.
Dk.Mwegoha alisema mboga zilizomwagiwa maji hayo zilibainika kuwa na
sumu zilizokuwa na madini ya risasi,shaba na kromiamu ambazo zote zina
madhara kwa binadamu.
Aliasema katika utafiti huo walibaini kuwa mboga hizo zinauzwa kwenye
masoko ya Ilala, Kariakoo, Buguruni, Veterani,Tazara, Mwananyamala,
Mnyamani, Kigogo, Kisutu, Vingunguti, Tabata, Mikoroshini na maeneo ya
jirani na wkaulima hao.
Chanzo: Nipashe
0 comments:
Post a Comment