Sunday, December 28, 2014

DIAMOND PLATNUMZ NA VANNESA MDEE WASHINDA TUZO ZA AFRIMA, NIGERIA *PICHAZ*



WANAMUZIKI wa Bongo falvour nchini Daimond Platnumz na vannesa Mdee wameshinda tuzo kubwa za muziki zilizofanyika nchini Nigeria maarufu kama Afrima.
Tuzo hizo zilizotolewa dec 27 zilihusisha wanamuziki kutoka kanda za bara la Afrika waliofanya vizuri katika kipindi chote cha mwaka 2014.
kupitia wimbo wake wa come over mwanamuziki Vannesa mdee ameshinda kipengele cha msanii bora wa kike Afrika mashariki na kuwashinda baadhi ya wasanii kama Wahu, kaz na size 8 wote kutoka nchini Kenya.
Diamond na Davido.
Lakini kwa upande wake Diamond ameshinda tunzo ya msanii bora wa kiume kwa kuwapiku wasanii maarufu kama Jose Chameleone na kidumu kupitia wimbo wake maarufu wa number one.
Vanessa akaandika hivi katika ukurasa wake:
“To God be the Glory, ThankYou soo much for voting - I love you #BestFemaleEastAfrica #Tanzania”
Wasanii wengine waliofanikiwa kushinda tunzo hizo ni pamoja na Davido aliyeondoka na tunzo ya msanii bora wa mwaka huku mwanamuziki 2face, Radio na weasel, pamoja na  Elan kutoka kenya wote wakiondoka na tunzo moja moja.
Mbali na Wasanii hao, pia Tanzania iliwakilishwa na mwanamuziki Peter Msechu ambae hakufanikiwa kushinda tunzo hizo.
Diamond na Vanessa Mdee wote waliteuliwa kuwania katika vipengele viwili na kubahatika tunzo moja kila mtu.
Hongera Diamond na Vee money.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI