Baadhi ya washiriki wa warsha ya utambuzi wa kaya maskini inayoendeshwa na TASAF.
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF unaendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo wawezeshaji wa utambuzi wa kaya maskini katika halmashauri kadhaa nchini. Zoezi hilo ni mwendelezo wa jitihada za TASAF za kunusuru kaya maskini nchini zoezi lililoanza mwaka uliopita kwa awamu katika maeneo mbalimbali nchini.
Miongoni mwa halmashauri ambako mafunzo hayo yanafanyika ni wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa ambako wawezeshaji hao watashiriki katika kuwapa mafunzo wadodosaji watakaofanya kazi ya tathmini itakayowezesha kutambua kaya maskini katika vijiji vipatavyo 94.
Baadhi ya washiriki wa warsha ya utambuzi wa kaya maskini katika eneo la utekelezaji la wilaya ya Mufindi wakimskiliza mwezeshaji wa warsha (hayupo pichani).
Mmoja wa wawezeshaji katika warsha ya kuwajengea uelewa wawezeshaji ngazi ya halmashauri ya wilaya ya Mufindi akiwasilisha mada.
Mtaalamu wa ushauri wa TASAF katika halmashauri ya wilaya ya Mufindi ,Lawrence Mwakitalu akitoa mada kwenye warsha ya kuwajengea uelewa wawezeshaji wa ngazi ya halmashauri ya wilaya ya Mufindi.
washiriki wa warsha ya utambuzi wa kaya maskini katika wilaya ya Mufindi mkoani Iirnga wakimsikiliza mwezeshaji wa warsha hayupo pichani.
0 comments:
Post a Comment