Sergio Aguero akishangilia baada ya kuifungia Man City bao pekee, huku wachezaji wa Manchester United wakiwa wameduwaa.
BAO pekee la Sergio Aguero jana jioni limeipa ushindi mwembamba wa 1-0 Manchester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Etihad dhidi ya mahasimu, Manchester United.
Aguero alifunga bao hilo dakika ya 63 akimfunga kipa wa United, David de Gea ambaye timu yake ilichea pungufu tangu dakika ya 39, baada ya Chris Smalling alipotolewa kwa kadi nyekundu. Beki mwingine wa United, Marcos Rojo alitolewa nje kwa machela baada ya kuumia bega.
Kikosi cha Manchester City kilikuwa: Hart, Zabaleta, Kompany, Demichelis, Clichy, Navas, Toure, Fernando, Milner/Nasri dk70, Aguero/Fernandinho dk83 na Jovetic/Dzeko dk71.
Manchester United: De Gea, Valencia, Smalling, Rojo/McNair dk56, Shaw, Fellaini, Blind, Rooney, Januzaj/Carrick dk43, Van Persie/Wilson dk82 na Di Maria.
0 comments:
Post a Comment