JOKATE MWEGELO ni mwanamitindo, msani, mtangazaji na mshereheshaji katika hafla mbali mbali za kitaifa, mwanadada huyu amezidi kukua katika tasnia hii ya burudani na utangazaji umemfanya azidi kukua maradufu.
Akiwa ni mtangazaji wa kipindi cha The one show ambacho kinarushwa kupitia runinga ya TV One anachoshirikiana na Ezden 'The Rocker', hivi karibuni inasemekana amepata Dili na DSTV kufanya kipindi kitakachokuwa kikirushwa na moja ya chanel zake.
Kwa kutuhakikishia hilo watanzania, mwanadada huyu amepost katika ukurasa wake wa instagram akideclare kuwa kuna show mpya inakuja..!
Mashabiki wange wengi wamekuwa na shauku ya kuona na kuifahamu show hiyo, huku mwenyewe akionekana kama anataka iwe ni sapraizi kwa mashabiki wake.
Haayaa yetu macho tuu.
0 comments:
Post a Comment