Anaitwa Chris Walton na pia kimuziki anaitwa `The Duchess` ndie alieingia kwenye kitabu cha rekodi za dunia cha Guinness Book of World Record kama mwanamke mwenye kucha ndefu kuliko wote duniani kwa sasa.
Inasemwa kuwa unapokutana na mwanadada huyo hakuna jinsi bali ni kumwangalia kwa mshangao,lakini angalau kucha zake ni safi na zinang`arishwa kwa dawa maalum
Anaweza akachukuliwa kama mchafu kwa kuwa hajazikata kwa miaka 20 lakini mrembo huyo mwenyeji wa Las Vegas kwa Obama,amewavuta watu wa Guinness World Book of Record.The Duchess ni muimbaji anaechipukia kwenye fani kwa sasa.
Awali mwanamama Lee Redmond ndie aliekuwa akiongoza kwa kushikilia rekodi ya kuwa na kucha ndefu kuliko wote ambazo zilifikia urefu wa futi 28 kabla hazijavunjika katika ajali ya gari mwaka 2011.
Kabla ya ajali, Bi Redmond hakuwahi kukata kucha za vidole vyake vya mkononi tangu mwaka 1979!
Bibi Lee Redmond |
0 comments:
Post a Comment