Sunday, November 2, 2014

DKT GHALIB MOHAMED BILAL AWATAKA WATENDAJI WA SERIKALI KUACHA URASIMU

Makamu wa Rais akiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajabu Ruketngwe kushoto kwa makamu wa Rais na Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manynya wakimwongoza kuelekea Banda la Mkoa wa Katavi kupata maelezo juu ya fursa za uwekezaji na maeneo ya uwekezaji katika mkoa huu na kukagua bidhaa za wajasiliamali katika kongamano la uwekezaji nalililoandamana na maonesho ya biashara ya SIDO yaliyofanyika mjini sumbawanga kwenye viwanja vya Nelson Mandelea Mkoa Rukwa.
Dkt Bilal akiwapungia mkono wananchi wa Mkoa wa Rukwa waliofika uwanjani kumpokea alipowasiri kufungua kongamano la uwekezaji Mjini Sumbawanga kwa mikoa ya ukanda wa ziwa Tangantika.akiongozwa na mwenyeji wake Mhandisi Stella Manyanya mkuu wa Mkoa wa Rukwa na mwenye Tsheti ya bluu bahari ni Dkt Mary Nagu waziri wa uwezeshaji na uwekezaji.
Hapo Dkt Bilal Makamu wa Rais akisalimiana na Viongozi mbalimbali waliofika kumlaki uwanjani hapo alipowasiri kufungua kongamano la uwekezaji,
(Picha zote na Kibada Kibada -Rukwa)
***********
Na Kibada Kibada –Rukwa
Makamu wa Rais Dkt Ghalib Mohamed Bilal amewataka wale wote walio katika ngazi za madaraka Serikali na kwenye mamlaka mbalimbali za maamuzi kuacha urasimu katika kutoa ushirikiano kwa wawekezaji wanapoonesha nia ya kuja kuwekeza katika Tanzania.
Dkt Bilal alitoa agizo hilo wakati akifungua Kongamano la Uwekezaji kwa mikoa ya Rukwa Katavi na Kigoma liliofanyika Mjini Sumbawanga kwenye uwanja wa Nelson Mandela Mkoani Rukwa.
Amesema watu wamekuwa na mitazamo hasi katika sekta ya uwekezaji na vitega uchumi,akasema katika uchumi wa leo bila uwekezaji hakuna maendeleo,uwekezaji utasaidia katika kukuza uchumi,utasaidiakupunguza umasikini,kuongeza ajira katika nchi.
Dkt Bilal akaeleza kuwa uchumi katika dunia ya leo ni uwekezaji kwa kuwa hata nchi ya China ambayo uchumi wake ni wa pili kwa ukuaji duniani bado inakaribisha wawekezajij,sasa itakuwa jambo la ajambo kwa nchi kama Tanzania kuwakataa wawekezaji kuja kukuza uchumi kwa kuwekeza katika sekta mbalimbali.
Dkt Bilal akawahimiza wananchi wenye uwezo kujitokeza kuwekeza katika fursa mbalimbali zilizopo katika ukanda wa Mikoa hii ya Ziwa Tanganyika.
Akazihimiza halamashauri kutenga maeneo ya uwekezaji na kufungua milango ya uwekezaji kwa kuondoa urasimu usiokuwa wa lazima watoe ushirikiano wa karibu kwa wawekezaji wanapojitokeza kuwekeza katika mkoa mikoa hiyo.
Kila mmoja kwa nafasi yake atoe ushirikiano wa karibu kila mmoja awajibike kwa nafasi yake kwa kuwa ana mchango mkubwa wa uwekezaji katika ukanda huu.
Awali Waziri wa Uwezeshaji na uwekezaji Dkt Mary Nagu kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais kufungua kongamano hilo alieleza kuwa Serikali imeweka mazingira mazuri ya uwezeshaji kwa ajili ya kurahisisha uwekezaji katika ukanda huu wa ziwa Tanganyika
Akizungumzia fursa zilizopo za uwekezaji katika ukanda wa ziwa Tanganyika amewahimiza watu wajitokeza kuwekeza katika ukanda wa mikoa hiyo kwa kuwa mazingira ya uwekezaji ni rafiki kwa kuwa sasa ukanda huu unafikika kwa urahisi kwa kutumia usafi wa anga na barabara kwa kuwa miundo mbinu ya barabra imefunguka.
Kwa hiyo kazi iliyopo ni kuimarisha uchumi wa nchi na hasa ukanda huu wa ziwa Tanganyika ambao unafursa nyingi katika uwekezaji, akaeleza kuwa uendeshaji wa makongamano ni utaratibu uliowekwa na serikali kwa ajili ya kuwezesha makongamano kwenye kanda ambapo hadi sasa kikanda makongamano haya yamefanyika katika kanda za Kaskazini, Mashariki, ukanda wa Ziwa,Kusini na Kanda ya ziwa Tanganyika ambapo kote kuliko fanyika makongamano hayo kumeonesha mabadiliko makubwa ya kukua kwa uchumi.
Akasema nchi ya Tanzania inaongoza kwa nchi za Afrika Mashariki kwa kuwa na wawekezaji kuliko nchi nyingine za Afrika Mashariki,ambapo katika kipindi cha mwaka jana uwekezaji uliingia kiasi cha dola 1.87 milioni kwa mwaka jana,hata hivyo uwekezaji huo unaelekezwa katika miji ya Mwanza, Dar es Salaam, Arusha Pwani na Mbeya.
Awali wakuu wa Mikoa ya Rukwa Mhandisi Stela Manyanya, Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajabu Rutengwe,na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luteni Kanali Mstaafu Issa Salehe Machibya walielezea fursa zilizopo katika mikoa ya kuweza kuwekeza katika maeneo ya mikoa ya Ukanda wa Ziwa Tanganyika ambapo fursa zipo nyingi.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI