KUNDI la wanamgambo wa Boko Haram nchini Nigeria limekana madai kutoka kwa serikali ya Nigeria kuwa wamefikia makubaliano.
Kundi hili limeachia kanda mpya ya video inayowaonyesha wanamgambo wa boko haramu wakiwa kimya wamejipanga huku mbele akionekana kiongozi wa kundi hilo Aboubakar Shekau.
Kiongozi huyo wa kundi la Boko Haramu Abubakar Shekau anaanza kwa kukana kuwa hakuna majadiliano yoyote baina yao na serikali ya Nigeria. Huku akihoji makubaliano hayo yalifanyika wapi? kwani wao kiu yao sasa ni kupambana, kuvamia, kuuwa kwa bunduki na migomo.
Kiongozi huyo wa Boko Haramu pia alitumia ujumbe huo kuthibitisha kuwa wanamshikilia raia mmoja mjerumani ambaye anakisiwa kuwa mwalimu aliyetekwa nyara mwezi Julai.
Huku akicheka shekau anasema kuwa zaidi ya wasichana 200 waliotekwa nyara kutoka eneo la Chibok kaskazini mwa Nigeria wamebadili dini na kuwa waislamu na tayari wame waozesha na wapo kwenye ndoa zao.
Hata hivyo kanda hiyo inaisha huku ikimuonyesha shekau akiweka msisitizo kuwa hawajafanya makubaliano na nchi yoyote wala umoja wa mataifa na kuwa taarifa za makubaliano ni za uongo kwani hawana mpango wakufanya hivyo.
0 comments:
Post a Comment