Thursday, November 27, 2014

BILIONEA DANGOTE AKAGUA UJENZI WA KIWANDA CHAKE CHA SARUJI MTWARA *PICHAZ*

 Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Industries Group), mfanyabiashara maarufu Afrika, Alhaji Aliko Dangote akitumia gari kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda chake kikubwa cha saruji katika Kijiji cha Msijute, mkoani Mtwara.
 Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Industries Group), mfanyabiashara maarufu Afrika, Alhaji Aliko Dangote (kushoto) akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Dangote nchini, Esther Baruti kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara.
 Alhaji Aliko Dangote kutoka Nigeria, akilakiwa na Mwakilishi Mkazi wa Dangote nchini, Esther Baruti alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara.
 Balozi wa Nigeria nchini, Dk. Ishaya Manjanbu akimlaki Alhaji Dangote.
 Dangote akiwa na Mwakilishi Mkazi wa Kampuni yake hapa nchini, Esther Baruti
Dangote akikaribishwa na viongozi wa kampuni ya Dil & Sinoma alipowasili eneo la Kiwanda cha simenti cha Dangote.
 Alhaji Dangote akiwa na maofisa wake  katika kikao na viongozi wa kampuni inayojenga kiwanda hicho ya Dil & Sinoma kwa ajili ya kupewa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho ambacho kitakuwa cha tatu kwa ukubwa Afrika.
 Waandishi wa habari wakimhoji Dangote kuhusu maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho
Alhaji Aliko Dangote akiongea na waandishi wa habari.
 Alhaji Dangote akiwa kwenye msafara wa magari akikagua maendeleo ya ujenzi ya kiwanda cha saruji Mtwara.
 Mwakilishi Mkazi wa Kampuni hiyo ya Dangote hapa nchini, Esther Baruti akiwa na mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni ya Dangote.
 Alhaji Dangote akisindikizwa kwenda kupanda ndege kwenda nchini Ethiopia kuendelea na ziara yake.
 Ofisa Mnadhimu wa Poilisi Mkoa wa Mtwara, George Salala akiagana na Alhaji Dangote.
 Alhaji Dangote akipanda ndege tayari kuondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara.
 Mwakilishi Mkazi wa Dangote hapa nchini, Esther Baruti akiondoka baada ya kuagana na Dangote.
Ndege iliyombeba Alhaji Dangote ikipaa.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI