MFANYAKAZI wa Umoja wa mataifa aliesafirishwa mpaka Ujerumani akitokea Liberia
wiki iliyopita baada ya kupatwa na virusi vya ugonjwa wa Ebola,
amefariki dunia kwenye hospitali ya St. Georg Ujerumani.Kifo chake
kinamfanya kuwa binadamu wa kwanza kufariki kwa Ebola ndani ya ardhi ya
Ujerumani ambapo Mwanaume huyu raia wa Sudan mwenye umri wa miaka 56
alifikishwa kwenye hospitali hiyo akiwa na hali mbaya ambapo amefariki
jana usiku baada ya hali yake kuwa mbaya pamoja na kwamba alipewa
uangalizi mkubwa wa kupatiwa matibabu.
Kuna hii stori ya shirika la afya la umoja wa mataifa kwamba karibu
watu 8,400 waliathirika na gonjwa la ebola ambapo 4,000 kati yao
wamefariki.
Msudan huyu aliefariki dunia anakuwa mgonjwa wa tatu wa Ebola
kutibiwa nchini Ujerumani sababu tayari kuna Mganda mmoja daktari amekua
akitibiwa huko Frankfurt, wakati Yule Msenegal aliruhusiwa kutoka
hospitali hivi karibuni baada ya kutibiwa kwa wiki tano.
0 comments:
Post a Comment