Saturday, October 4, 2014

TAARIFA YA BALOZI WA TANZANIA CHINA KUWATISHIA WAFUNGWA WA MADAWA YA KULEVYA WALIOKAMATWA CHINA

GAZETI la South China Morning Post linadai kuwa Balozi wa Tanzania nchini China Luteni Generali mstaafu Abdulrahman Shimbo amewatishia wafungwa wa Kitanzania walioko magerezani Hong Kong kwa kupatikana na hatia ya kusafirisha madawa ya kulevya nchi humo. 
Balozi Shimbo anadaiwa kuwaonya wafungwa hao kuwa familia zao nchini Tanzania zitakuwa hatarini kama wafungwa hao wataendelea na kampeni yao ya kuwaonya Watanzania wengine kutojihusisha na biashara ya madawa ya kulevya.
Mwezi uliopita Balozi Shimbo alifanya zaira katika gereza la Stanley nchini Hong Kong. 
"Ziara ya balozi wetu ilikuwa kama janga kwetu" alisema Gervas, ambaye ni moja ya wafungwa katika gereza la Stanely." Gervas aliongeza 
"Ametukatisha tamaa katika kampeni yetu dhidi ya madawa ya kulevya, ikiwa ni pamoja na kututahadharisha kuwa tuwe makini au tutahatarisha maisha ya familia zetu Tanzania. Pia Balozi Shimbo alienda mabli zaidi na kukosoa kampeni zetu akisema kuwa hazijaleta mabadiliko makubwa".
Hata hivyo, Edmund Kitokezi, ambaye ni afisa katika Ubalozi wa Tanzania uliopo jijini Beijing, amekanusha kuwa Balozi Shimbo amewatishia wafungwa hao na kuongeza kuwa badala yake Balozi aliwapa moyo wa kufunguka zaidi. 
"Tunaunga mkono kampeni yao - hii ndiyo position ya serikali. Siyo kazi ya ubalozi kumwambia kila mtu aachane na hiyo kampeni" alisema Kotokezi.
Watanzania waliofungwa Hong Kong walianza kampeni yao dhidi ya biashara ya madawa ya kulevya kwa kuandika barua ambazo zimekuwa zikichapishwa na Padri Fr John Wotherspoon katika tovuti yake  Padri Wotherspoon anatoa huduma za kiimani katika magereza huko Hong Kong.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI