Nyota
wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ akifanya shoo ndani ya Ukumbi wa
Matei Lounge mjini Dodoma. Aibu hiyo ilimkuta staa huyo ndani ya Ukumbi
wa Matei Lounge mjini Dodoma ambako sukari huyo wa warembo alikuwa
akifanya shoo.
*************
KWELI ni
aibu nyingine! Nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ Jumamosi
iliyopita alikumbwa na aibu nyingine kufuatia onesho lake kufanyika
ndivyo sivyo na hivyo kuzua tafrani miongoni mwa mashabiki wake mjini
hapa.
Aibu yenyewe iliyompata Diamond ilisababishwa na kuzimika kwa muziki
wake mara tatu katika onesho hilo na hivyo kuwafanya mashabiki kupiga
kelele hukuwengine wakidai pesa zao za viingilio.
Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiendelea na shoo. MAFUNDI MITAMBO WAHAHA
Hali hiyo iliwafanya mafundi mitambo kurekebisha nyaya kwa zaidi ya
dakika 20 kila pale muziki ulipozimika hali iliyosababisha watu kuzidi
kupiga mayowe na kumtolea maneno ya shombo Diamond, wengine wakitishia
kumpopoa kwa mawe.
Muda mfupi baada ya mitambo hiyo kurekebishwa, mashabiki walianza
kuserebuka tena lakini baada ya dakika 45 muziki ulizima tena na
kusababisha mayowe mengine ya mashabiki wakiendelea kusema wameliwa pesa
zao.
Mafundi mitambo wakirekebisha nyaya ili shoo iendelee.
WEMA ATAKIWA
Katika zomeazomea ya safari hii, mashabiki walikwenda mbele zaidi
wakimtaka Wema apande jukwaani kusalimia wakati mitambo ikirekebishwa
wakiamini Diamond alikwenda na bebi wake huyo kwenye onesho hilo.
Hata hivyo, mafundi mitambo waliingia tena kibaruani na kurekebisha mambo baada ya dakika 23 muziki ukaendelea.
MAIKI NAZO ZAKOROMA
Diamond alianza kufanya tena makamuzi ndipo maiki nazo zikaanza
kukoroma ambapo alianza kuwaomba wasaidizi wake wambabidilishie lakini
kila waliyompa ilikuwa ikikoroma na kuwafanya mashabiki wazidi kupandwa
na hasira.
Mashabiki
wakisubiri shoo ilipobuma. Kitendo hicho kilimfanya Diamond asimamishe
onesho na kuanza kumtupia lawama muandaaji (Matei) akidai kuwa
ameshindwa kuweka hata betri mpya kwenye maiki alizomuandalia wakati
amewatoza mashabiki kiingilio kikubwa cha shilingi 35,000 (kawaida) na
40,000 kwa VIP.
“Haiwezekani bwana, huu ni ubabaishaji wa hali ya juu, mwandaaji gani
unaandaa shoo, unawachaji mashabiki kiingilio kikubwa halafu unashindwa
hata kuweka betri mpya kwenye maiki?
Nasibu Abdul ‘Diamond’ akisubiriri mitambo ikae sawa.
DIAMOND ABANWA NA RISASI JUMATANO
Kufuatia hali hiyo, baada ya shoo, Risasi Jumatano lilimfuata Diamond
na kumuuliza kulikoni muziki wake kuwa mwepesi pia kukatikakatika kila
mara hukumaiki nazo zikikoroma.
“Braza huu muziki siyo kabisa, huu ni muziki wa kupiga kwenye
vigodoro lakini siyo wa kufanyia shoo zangu hasa kama hii ambayo watu
wameingia kwa bei mbaya, ni kuwaibia watu.
“Mimi ni mtoto wa Kiislam ni lazima niongee ukweli, niliposikia
sehemu yenyewe ninayokuja kufanyia shoo inaitwa Matei Lounge nikajua ni
sehemu bab’ kubwa lakini kumbe ni ubabaishaji mtupu,” alilalama Diamond.
Nasibu Abdul ‘Diamond’ akirejea kuendelea na shoo.
INTAVYUU FUPI
Katika intavyuu fupi, Diamond, alisema anadhani kama anahujumiwa
kwani haiwezekani muandaaji ashindwe kuweka vitu muhimu kwenye shoo.
alidai wanafanya hivyo wakijua inapotokea tatizo kama hilo anayejulikana
ni Diamond.
UJERUMANI, UINGEREZA
Ilianza nchini Ujerumani ambapo staa huyo alinusurika kudundwa
kufuatia vurugu zilizoibuka ukumbini alfajiri ya Jumapili ya Agosti 31,
mwaka huu baada ya kucheleweshwa kupanda stejini kwenye Ukumbi wa
Sindelfingen uliopo Mji wa Stuttgart.
Nasibu
Abdul ‘Diamond’ akitoa burudani. Nchini Uingereza nako, Septemba 20,
mwaka huu, Diamond alijikuta ndani ya aibu kubwa kwa mashabiki wake
kufuatia mwandaaji kuingia mitini katika ukumbi wa LafACE club jijini
Londan licha ya mashabiki kujaa.
KASORO YA DAIMOND NI MAMBO YA ‘USWAHILI’
Uchunguzi wa gazeti hili umegundua kuwa, Diamond licha ya kuwa msanii
mkubwa kwa sasa lakini bado anaendesha mambo yake ‘kiswahili’ sana.
Nuhu
Mziwanda na bebi wake Shilole wakitoa sapoti katika shoo ya Diamond.
Kwa kawaida, msanii anapokwenda kupiga shoo mahali, kuna utaratibu
unaoitwa kwa Kiingereza kama Technical Rider ambapo wasimamizi wake,
akiwemo meneja huenda kuukagua ukumbi, usalama, muziki wenye viwango na
hata steji shoo ilivyo.
Kama mambo hayo hayatakuwepo, msanii anaweza kugoma kufanya shoo.
Lakini mambo yote hayo hutakiwa kuwepo kwenye mkataba wa
makubaliano.Meneja wa Diamond, Babu Tale alipopigiwa simu juzi ili
kuulizwa kwa nini hakuwepo Dodoma kuhakikisha uwezo wa vyombo vya muziki
na maandalizi mengine, hakupatikana hewani!
Chanzo: GP
0 comments:
Post a Comment