Wednesday, October 1, 2014

SHIRIKISHO LA SOKA LA NIGERIA 'NFF' LAPATA RAIS MPYA

Amaju Pinnick amechaguliwa kuwa rais mpya wa NFF. 
SHIRIKISHO la soka la Nigeria (NFF) limemchagua Amaju Pinnick kama rais wake mpya baada ya kupiga kura siku ya Jumanne.
Pinnick, 43, ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya Delta State Commission, mkuu wa Delta FA na mwenyekiti wa Warri Wolves, alipata kura 32 kati ya 44 zilizopigwa katika hatua pili ya upigaji kura.
Mahasimu Dominic Iorfa alipata kura nane na Taiwo Ogunjobi akaambulia nne.
Hata hivyo, mtu aliyeaminiwa kuwa mgombea wa kwanza wa kazi hiyo, Shehu Dikko, alijitoa kwenye uchaguzi huo.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI