Mshambuliaji wa Albania, Bekim Balaj akipigwa na kiri kilichorushwa na shabiki wa Serbia.
MECHI ya kufuzu kwa Fainali za Euro
2016 baina ya Serbia na Albania ilivunjika baada ya dakika 30 usiku wa
jana, kufuatia beki wa Serbia, Stefan Mitrovic kuitupa bendera ya
Albania na kusababisha Uwanja wa Partizan, mjini Belgrade kugeuka sehemu
ya mapambano.
Shabiki akimpiga ngumi mchezaji wa Albania, Mergim Mavraj.
UEFA iliwafungia mashabiki wa Albania kuhudhuria mechi hiyo ya Kundi I mjini Belgrade, lakini iliruhusu nchi hizo mbili kumenyana, licha ya uhasama wa muda mrefu wa kisiasa baina yao.
Na wakati bendera
ya Albania iliyoambatana na ramani ya Kosovo na ujumbe wa
'autochthonous', wenye kumaanisha asili- ikipeperushwa juu ya eneo la
kuchezea kwa kutumia rimoti, kitendo cha Mitrovic kuirukia na kuitupa
kilisababisha balaa, wachezaji kwa wachezaji na mashabiki kuanza
kupigana.
0 comments:
Post a Comment