Klabu za Bayern Munich, Chelsea pamoja na Shakhtar Donetsk zimeweka rekodi ya kufunga mabao mengi katika nusu ya kwanza ya michezo ya hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Klabu
hizo tatu zimefanya hivyo usiku wa kuamkia hii leo katika michezo ya
mzunguuko wa tatu ambapo FC Bayern Munich walikuwa ugenini mjini Roma
nchini Italia, wakipambana na AS Roma ilihali Shakhtar Donetsk walikuwa
nyumbani mjini Donetsk nchini Ukraine wakicheza dhidi ya BATE Borisove
huku Chelsea wakicheza nyumbani Stamford Bridge dhidi ya NK Maribor
kutoka nchini Slovenia.FC
Bayern Munich pamoja na Shakhtar Donetsk ziilifanikiwa kuacha vilio kwa
wapinzani wao kufuatia ushindi wa mabao saba waliouvuna na kwa upande w
a
Chelsea waliibuka na ushindi wa mabao sita kwa sifuri na hivyo
kuendelea kujiweka katika mazingira mazuri ya kuichungulia nafasi ya
kutinga katika hatua ya 16 bora ya michuano ya ligi ya abingwa barani
Ulaya msimu huu.
Katika
mchezo wa FC Bayern Munich dhidi ya AS Roma mabao ya mabingwa hao
kutoka nchini Ujerumani yalifungwa na Mario Goetze, Robert Lewandowski,
Thomas Mueller, Xherdan Shaqiri, Franck Ribery pamoja na Arjen Robben
aliyefunga mabao mawili.
Bao
la AS Roma katika mchezo huo lilipachikwa wavuni na mshambuliaji kutoka
nyumbani Afrika katika nchi ya Ivory Coast Gervais Yao Kouassi
Gervinho.
Kwa
upande wa Shakhtar Donetsk mabao yao yalifungwa na Alex Teixeira,
Douglas Costa pamoja na Luiz Adriano aliyefunga mabao matano.
Chelsea
mabao yao yalipachikwa wavuni na Loic Remy, Didier Drogba, John Terry
pamoja na Eden Hazard aliefumnga mabao mawili huku Mitja Viler
akijifunga mwenyewe.
Matokeo ya michezo mingine ya ligi ya mabingwa barani Ulaya iliyochezwa usiku wa kuamkia hii leo ni kwamba
Schalke 04 4 - 3 Sporting CP
FC Porto 2 - 1 Athletic Bilbao
APOEL Nicosia 0 - 1 Paris Saint Germain
Barcelona 3 - 1 Ajax
CSKA Moscow 2 - 2 Manchester City
0 comments:
Post a Comment