Saturday, October 18, 2014

RAYUU: NIMEPIMA HAYA NA HUYO WOLPER NAYE AKAPIME UKIMWI… FUATILIA MKASA MZIMA HAPA!

MSANII wa filamu Bongo, Alice Bagenzi ‘Rayuu’ amemtaka msanii mwenzake, Jacqueline Wolper apime Ukimwi kama alivyofanya yeye. 
 Akiongea  na  mwandishi wetu, Rayuu alisema anamheshimu Wolper na kamwe hawezi kumsema vibaya lakini alishangaa kuambiwa na mashosti wake kwamba anamsema yeye ana Ukimwi. 
“Nilishangaa sana kwa kweli hilo jambo liliniumiza roho na linaniuma mpaka kesho, eti anawaambia watu mimi ni muathirika, lini alinipima au ana uthibitisho gani na hilo,” alisema Rayuu na kuongeza:
 “Kutokana na kunikosesha raha kwa kiasi kikubwa kwa jambo hilo, niliangua kilio nikaamua kwenda kupima na kuyaanika majibu yangu kwenye Istagram ili aumbuke kwa kuwa nipo safi, kama na yeye anaweza, akapime tuone majibu yake.”

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI