Rais wa jamuhuri ya muungano wa
Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete na rais wa serikali ya mapinduzi ya
Zanzibar Dk Ally Mohamed Shein wamekabidhiwa katiba iliyopendekezwa na
bunge maalum la katiba ikiwa ni hatua muhimu katika historia ya Tanzania
kuelekea kupata katiba mpya ambayo kwa mara ya kwanza imehusisha maoni
ya wananchi, makundi maalum, taasisi wanasiasa na viongozi mbalimbali
tangu taifa kupata uhuru wake.
Majira ya saa sita na nusu mchana ndipo makundi mbalimbali ya
wageni waalikwa, viongozi wa juu wa serikali mabalozi marais na mawaziri
wa kuu wastaafu wakaingia katika viwanja vya jamuhuri na kisha majira
ya saa tisa na nusu rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Dk Ally
Mohamed Shein akawasili na kufuatiwa na rais wa jamuhuri ya muungano wa
Tanzania.
Mara baada ya itifaki ya uongozi kuwasili shughuli ikaanza rasmi
ambapo mwenyekiti wa kamati ya uandishi ya bunge maalum Mhe Adrew Chenge
akaelezea maudhui ya katiba iliyopendekezwa pamoja na mambo mengine
akasema katiba hiyo ina jumla ya sura 19 na ibara 296 na nyongeza tatu
ambapo rasimu ya awali iliyowasilishwa bungeni ilikuwa na sura 17 na
ibara 211 huku suala la muundo wa serikali likisalia kuwa serikali
mbili.
Nao wawakilishi wa makundi 15 ya kijamii yalisyoshiriki katika
bunge hilo maalum la katiba walipata fursa ya kuelezea namna
walivyowakilisha na kile walichokubaliana kiwepo katika katiba mpya.
Na kisha kile ambacho kilikuwa kikisubiriwa katika hastoria ya
taifa kikawadia ambapo aliyekuwa mwenyekiti wa bunge maalum akakabidhi
rasimu ya katiba iliyopendekezwa kwa rais wa jamuhuri Dk Jakaya Kikwete
na rais wa Zanzibar Dk Ally Muhamad Shein.
Baada ya makabidhiano hayo viongozi hao wakuu wa taifa kuhusu
mchakato wa katiba ambapo wameelezea matumaini yao makubwa kuhusu katiba
hiyo pendekezwa.
Nao baadhi ya wanachi waliohudhuria siku hii hadhimu kwa
mustakabali wa taifa walikuwa walitoa maoni yao kuhusu mchakato mzima wa
uundwaji wa katiba mpya huku wakiwataka watanzania kuwa watulivu katika
kipindi chote na watumie vizuri kura ya maoni ili kupata katiba
itakayokuwa mwarubaini wa kutatua changamoto zinazolikabili taifa na
yenye mrego wa kimaendeleo.
Chanzo: ITV HABARI
0 comments:
Post a Comment