Jon Schultz
MFANYABIASHARA
mmoja ameamua kutumia ‘fursa’ aliyoiona kupitia janga la Ebola
linalosumbua maeneo mbalimbali ya dunia kwa sasa, kwa kuuza domain ya
www.ebola.com kwa pesa nyingi.
Jamaa
huyo anayejiita ‘domain entrepreneur’ aliinunua domain hiyo miaka minne
iliyopita (2008) kwa $13,500 sawa na zaidi ya shilingi milioni 22, na
amedai kuwa alikuwa akisubiri wakati muafaka wa kuiuza.
“Ebola.com
would be a great domain for a pharmaceutical company working on a
vaccine or cure, a company selling pandemic or disaster-preparedness
supplies, or a medical company wishing to provide information and
advertise services” Schultz aliiambia CNBC.
Kwa
mujibu wa Daily Mail, Schultz piz anamiliki domain zingine kama
H1N1.com, birdflu.com, terror.com, PotassiumIodide.com, fukushima.com.
0 comments:
Post a Comment