Saturday, October 18, 2014

MAMBO YA KIGOMA HAYO: KUNA MIMEA AMBAYO INATIBU MAMBO MENGI KWA WANAUME!

WASWAHILI husema mtu hasahau asili. Barani Afrika kuna mimea mbalimbali ambayo bado inatumika kwa ajili ya matibabu, licha ya mingine mingi kutumika kama chakula. 
Hivi karibuni, mwandishi wa BBC Zuhura Yunus alikuwa mkoani Kigoma nchini Tanzania.
Katika pita pita yake alikutana na mmea ambao awali, kwa kuutazama alidhania ni mbuyu. 
Hata hivyo, alipozungumza na wenyeji wa eneo hilo linalojulikana kama Kabwe, akaelezwa mmea huo unaitwa Mlemela. Nini kilimvutia mwandishi wetu hata kuufuatilia mmea huo? Zuhura alifanya mahojiano na mkazi wa Kigoma, Birangwa Musa ambaye alimueleza kuwa mmea huo unatumika kwa matibabu hasa kwa wanaume. Kwanini wanaume?

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI