KATIKA nyumba tunazoishi mara
nyingi tumekua tukifuga na kuishi na Paka au Mbwa kitu ambacho ni kawaida na ni
nadra sana kukutana na mtu anaeishi na au kufuga viumbe ambavyo ni hatari kwa
maisha ya binadamu mfano Nyoka.
Sasa hii inaweza kutushangaza kwa sababu kuna Simba ajulikanaye kama mkuu
wa msitu alihamishia makazi yake kwenye nyumba ya Melanie Griffith mwigizaji
ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 57.
Unaambiwa Simba huyu alihamia kwenye nyumba hiyo toka Melanie akiwa na
umri wa miaka 14 huko Sherman Oaks,California Marekani ambapo mama yake Melanie
ni mwigizaji Tippi Hedren na baba yake wa kambo kwa muda huo Noel Marshall.
Kingine cha kufahamu ni kwamba hii familia ilikuwa inamlea Simba huyu
nyumbani ambae alipewa jina la Neil kama wanyama wengine, mfano Mbwa au Paka.
Picha za Melanie na mama yake wakiwa wanacheza na simba huyo ziliwekwa
kwenye jarida la ‘Life Magazine‘ mwaka 1971 ambapo
zilikua zinaonesha mtoto huyo kuwa na ukaribu mkubwa na Simba na hata kulala na
kuogelea nae.
Mama Melanie aliyeigiza kwenye filamu ya ‘The Birds’ miaka 8
baada ya kupigwa kwa picha hizo alionekana pia kupenda kucheza na mnyama huyo
pori.
Simba huyu alikuja kuishi na familia hiyo wakati mama Melanie na baba
wakiwa wanatengeneza filamu Afrika ambapo kwenye matembezi yao waliona kuna
nyumba yenye Simba ambao hawana makazi mazuri ndipo walipoamua kumchukua Simba
huyo kutengeneza filamu inayohusiana na Simba.
Kweli baadae walitengeza filamu iliyoitwa ‘Roar’ ambapo ilitolewa kwenye
miaka ya 80 ambapo kwenye mahojiano yaliyofanywa mwezi April mwaka 1982 na The
Guardian, U.K ilitangazwa filamu hiyo ya Roar.
Griffith alielezea jinsi alivyopata alama za usoni na kusema Simba huyo
hakumaanisha kumuumiza, aliendelea kusema ‘Baada ya kukaa miaka 7 na Simba
unasahau kama Simba ni mnyama na pia ni hatari kuwa nao karibu, katika
utengenezaji wa filamu hamna mnyama alieumia sema watengenezaji wengi wameumia
na wapo hospitali’
Mama wa Griffith ambaye sasa ana miaka 85 alipendezwa sana na uhusiano wa
Griffith na wanyama mpaka akaamua afungue kituo cha kulea wanyama ambao
wamekosa malezi kiitwacho ‘Shambala Preserve’ kwenye mjia wa Acton
California Marekani mwaka 1972.
0 comments:
Post a Comment