Sunday, October 5, 2014

BAWACHA WALIPOANDAMANA KUELEKEA IKULU, NA HALIMA MDEE KUKAMATWA NA POLISI *PICHAZ*


 Mwenyekiti  wa BAWACHA ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Kawe kupitia CHADEMA Halima Mdee akiwa katika maandamano akiwaongoza wanawake wenzake kuelekea Ikulu kumpelekea ujumbe Rais Jakaya Kikwete kwamba hasikubali kuweka saini Rasimu mpya iliyopitishwa juzi mjini Dodoma, maandamano hayo kabla hayajafika mbali walitawanywa na jeshi la polisi lililotumia maji ya kuwasha pamoja na kupigwa kwa waandamanaji na kumshika mwenyekiti huyo Halima Mdee pamoja na wafuasi wake na kupelekwa polisi Osterbay.
 
Polisi  wakimpandisha Halima mdee kwenye gari la polisi.
 
Mfuasi wa chadema akishikiliwa na polisi na kupelekwa katika gari la polisi
 


 
Halima Mdee akiwa ndani ya gari la polisi pamoja na wafuasi wa chadema wakipelekwa katika kituo cha polisi cha Osterbay.
 
Halima mdee akizozana  na polisi mara baada ya kuingizwa kwenye gari
Wafuasi wa chadema wakimueleza polisi madai yao wakiwa nje ya kituo cha polisi cha Osterbay wakidai kwenda kwa wanaohusika kutuoni hapo kwa ajili ya kumtoa mwenyekiti wao Halima Mndee.
 
 
Wafuasi wa chadema wakilalamika  kwa polisi
 
Kituo cha polisi cha Osterbay kilikuwa na ulinzi wa kutosha na hakuruhusiwa mtu yeyote kuingia kituoni hapo.
 
Polisi wa Osterbay wakizuia gari kupitia
 
Wakina mama wa chadema wakifika katika eneo la polisi Osterbay.
 
 
Viongozi wa chadema wakiomba kuruhusiwa kupita polisi ya Osterbay.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI