IDADI ya watu waliokufa kwenye ghorofa la makao makuu ya Kanisa la SCOAN (Synagogue Church of All Nations) la Nabii TB Joshua wamefikia 50.
Jengo hilo la ghorofa tano ambalo ni makao makuu ya kanisa na nyumba ya kulala wageni iliporomoka Jumamosi wakati ujenzi ukiendelea.
Hadi kufikia Jumapili jumla ya watu 41 walikuwa wameripotiwa kufariki, lakini maiti nyingine tisa zimeongezeka.
Inaelezwa kwamba, mhubiri huyo wa kimataifa alipewa kibali cha kujenga ghorofa mbili, lakini mwenyewe akaamua kujenga ghorofa tano.
Uokoaji bado unaendelea na watu wengine 124 walikuwa wameokolewa wakiwa hai hadi kufikia Jumapili.
Mmoja wa majeruhi waliookolewa kwenye kanisa hilo akiwa hajitambui.
Jengo hilo liko katika eneo la Ikotun magharibi mwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Lagos.
LAGOS
0 comments:
Post a Comment