Tuesday, September 23, 2014

TUNDA MAN ALIPOSINDIKIZA SHOW YA VIPAJI VYA WAREMBO MISS TANZANIA, BABATI MKOANI MANYARA

 Warembo 15 kati ya 30 wanaoshiriki shindano la Redds Miss Tanzania 2014 wakisindikizwa na mkali wa Bongo Fleva kutoka Jijini Dar es Salaam, Tunda Man, wametoa burudani kali wakati wa shindano dogo la awali la kumtafuta mrembo mwenye kipaji lililofanyika Babati Mkoani Manyara. Pichani juu ni washindi wa tano waliofanikiwa kuingia fainali ya shindano hilo la vipaji litakalofanyika jijini Dar es Salaam baada ya wengine 15 kufanyika Arusha mjini.
 Warembo wenzao waliobakia wakishangilia burudani ya vipaji kutoka kwa washiriki wenzao.
 wadau wa sanaa ya Urembo Babati wakifuatilia shindano hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Christina Mndeme aliye mwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Manyara, akiwa na waratibu wa show hiyo, Mzee Ally Sumaye (kushoto) na Mfanyabiashara Mohamad Bajwa.
 Msanii wa Bongo Fleva  Tunda Man akitoa burudani kwa wadau wa urembo Babati.
 Tunda Man aliburudisha vilivyo ukumbini hapo.
 Jopo la majaji likifuatilia kwa makini shindano hilo

 Ilikuwa ni shwangwe kwa warembo hao ambao wapo Mikoa yua Kaskazini kwa ziara ya kimafunzo katika hifadhi za Taifa.
Chanzo Father Kidevu

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI