Saturday, September 6, 2014

TAMASHA LA FIESTA SASA KUFANYIKA KESHO JUMAPILI MJINI MUSOMA

MKURUGENZI wa uzalishaji na Vipindi, Bwa.Ruge Mutahaba kwa niaba ya uongozi wa Clouds Media Group na PrimeTime Promotions  Ltd ambao ndio waandaaji wa Tamasha la Fiesta 2014,ametangaza rasmi kuwa onesho la tamasha hilo lililobeba ujumbe murua kabisa wa sambaza upendo, litafanyika kesho jumapili ndani ya uwanja wa Karume.

Tamasha hilo la Fiesta lilipangwa kufanyika JANA ijumaa mjini Musoma mkoani Mara lakini kufuatia ajali mbaya iliyotokea mkoani humo jana na kusababisho vifo vya watu zaidi ya 40,iliyotokea katika kijiji cha Sabasaba, wilaya ya Butiama mkoani Mara lilisitishwa ili kwenda sambamba na tukio zima katika kuwafariji wakazi wa Musoma na vitongoji vyake, kutoa mkono wa pole. 

Wasanii waliotarajiwa kushiriki tamasha hilo na Waandaaji walitoa msaada wa vifaa tiba kwa hatua za awali kusaidia majeruhi waliokuwa wakipelekwa hospitali ya rufaa mjini Musoma.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI