Wednesday, September 10, 2014

TAHADHARI: TAARIFA MUHIMU KWA WATUMIAJI WA TIGO PESA!

Muonekano wa mojawapo ya link kutoka katika ujumbe wa email. 
Hii ni tahadhari kwa watumi
aji wa mitandao ya simu kuhusu utapeli ambao unaendelea kwa sasa ambapo kuna kundi la watu linatuma ujumbe mfupi kupitia simu za mkononi na barua pepe (email) zikiwataka watu kuhakiki akaunti zao. TAFADHALI USIFANYE HIVYO!
MOJAWAPO ya ujumbe kupitia barua pepe (email):
Ndugu customer,
Tusaidie kuweka akaunti yako salama.
Hivi karibu
ni, kumekuwa na kupanda kwa matukio ya usalama kwenye mtandao kuuliza wateja update huko Tigo pesa akaunti. Wakati tukiendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuweka mtandao wa Tigo pesa ya salama, Tunaomba watumiaji kutusaidia kuthibitisha akaunti zao na kuzifanya ziwe salama, tafadhali tembelea kiungo hiki kwa ajili ya uhakiki.
Regards, 
Tigo pesa66 Services ©
Ukibonyeza link hiyo ya 'kiungo hiki' utakutana na sehemu inayokutaka kuweka namba ya simu na neno la siri. USIFANYE HIVYO.
Mtandao huu umeongea na Msemaji wa kampuni ya Tigo Tanzania, John Wanyanja ambaye amethibitisha kuwa watu hao ni matapeli na wateja wao wasijaribu kuingiza taarifa zao!

0 comments:

Post a Comment